“ADF wanashukiwa kufanya mauaji haya” ambayo yamesababisha vifo vya watu ishirini na watatu miongoni mwa wakazi wa vijiji vya Lintumbe, Kisanga na Matuna, kwa mujibu wa taasisi inayofuatilia masuala ya usalama nchini DRC ambayo inaandika visa vya vurugu katika mikoa ya Kivu na Ituri.
Mwanaharakati wa eneo hilo, Christophe Munyanderu, pia ametoa tathmini hiyo hiyo, akiongeza kuwa baadhi ya waathiriwa waliuawa mashambani mwao.
Miongoni mwa makundi mengi yenye silaha yaliyopo mashariki mwa DRC, ADF (Allied Democratic Forces) wanatuhumiwa kuua maelfu ya raia katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.
Hapo awali kundi la waasi wa Uganda, ADF, lililoanzishwa nchini DRC tangu miaka ya 1990, lilitangaza utiifu wake mwaka 2019 kwa IS, ambayo inadai baadhi ya vitendo vyao na kulitangaza kama “tawi lake la Afrika ya Kati” (ISCAP kwa Kiingereza).
Uganda na DRC zilianzisha mashambulizi ya pamoja mwaka 2021 kuwatimua ADF katika ngome zake za Kongo, hadi sasa wameshindwa kukomesha mashambulizi ya kundi hilo.