CEO wa zamani wa Simba SC ambaye aliandika historia ya kuwa Mwanamke wa kwanza Tanzania kuwahi kushika nafasi ya juu ya Uongozi katika Club ya Simba SC leo ameitangaza good news.
Barbara ambaye alijiuzulu nafasi yake ya CEO Simba SC na kudaiwa kuendeleza maisha mengine ametangaza amepata mtoto na sasa yeye ni Mama J.
Taarifa hiyo Barbara ameitoa kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo amepost kwa kifupi tu kuandika New Mum halafu kwenye caption akaandika Mama J Alhamdullilah kwa Kila kitu.
Bado hajaweka wazi kirefu cha jina la mtoto wake lakini pia baba wa mtoto, Ayo TV inamtakia kila la kheri kwenye maisha mapya.