Rais wa Kenya, William Ruto leo amesema kesho asubuhi August 24,2023 atafanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa TikTok ili wakubaliane kwa pamoja jinsi ya kufanya usimamizi wa maudhui kwenye mtandao huo hii ni baada ya TikTok kulalamikiwa kukiuka maadili ya Wakenya.
Itakumbukwa hivi karibuni Bunge la Kenya lilipokea ombi la TikTok kupigwa marufuku nchini humo hii ni baada ya Wadau hao kusema jukwaa hilo linaongoza kwa uvunjaji wa kanuni ya faragha na kusambaza maudhui ya ngono.
Spika wa Bunge la Kenya, Moses Wetang’ula alisema ombi hilo liliwasilishwa na Mtu aitwaye Bob Ndolo akidai TikTok inakusanya taarifa muhimu kutoka kwa Watumiaji wake pamoja na kutumika lkuhamasisha vurugu, lugha chafu, kusambaza maudhui ya ngono na matamshi ya chuki.