Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy amefisia tangazo la uongozi wa Brics kuwa nchi yake itakuwa mwanachama wa muungano huo, hatua ambayo pia imepongezwa na nchi ya Iran.
Kupitia ukurasa wake wa X zamani ukijuliakana kama twitter, Abiy Ahamed amesema nchi yake iko tayari kushirkiana na mataifa mengine ya muungano huo katika ulingo wa kimataifa.
Kiongozi huyo aidha amesema hatua hii ni muhimu kwa raia wa nchi yake na kuwapongeza baada ya tangazo la Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa katika mkutano wa kilele wa BRICS kuwa nchi yao ni miongoni mwa nchi sita mpya zitazopata uanchama wa muungano huo.
Ethiopia, nchi ya pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika, itakuwa mwanachama kamili kuanzia Januari 1, 2024, pamoja na Argentina, Misri, Iran, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu.