Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen mwezi ujao atazuru Eswatini, mshirika wake pekee wa barani Afrika, wakati huu kiongozi huyo akijaribu kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.
Atahudhuria sherehe za kuadhimisha siku ya uhuru wa nchi na siku ya kuzaliwa kwa Mfalme Mswati III katika ziara hiyo.
Safari yake, kati ya tarehe 5 na 7 Septemba, itaadhimisha miaka 55 ya uhusiano wa nchi hizo mbili.
China inasema Taiwan ni sehemu yake na kwamba haina jukumu na kuwa na uhusiano na mataifa mengine.
Taiwan ina uhusiano rasmi na nchi 13 tu ikiwa ni pamoja na Eswatini.
Naibu waziri wa mambo ya nje wa Taiwan Roy Lee amenukuliwa akiwaambia waandishi wa habari kwamba ziara ya rais wa Taiwan si kushindana na ziara ya rais wa China Xi Jinping katika nchi jirani ya Afrika Kusini wiki hii.
Rais Tsai alitembelea Eswatini kwa mara ya mwisho mwaka wa 2018.
Ndiyo nchi pekee ya Afrika ambayo inadumisha uhusiano wa kidiplomasia na kisiwa hicho cha Asia baada ya Burkina Faso kuegemea upande wa China mwezi Mei 2018.