Matokeo ya kwanza ya maeneo bunge yalitangazwa siku ya Alhamisi katika uchaguzi wa Zimbabwe baada ya zoezi hilo kucheleweshwa, na hata kuongewewa muda katika baadhi ya vitongoji, huku wanaharakati wa asasi za kiraia wakikamatwa.

Raia wa Zimbabwe walimpigia kura rais, wabunge, na madiwani siku ya Jumatano, huku wengi wakielezea matumaini ya mabadiliko baada ya miaka mingi ya matatizo ya kiuchumi. Lakini wachambuzi walionya kuwa haiwezekani chama tawala cha ZANU-PF kuachia madaraka amabyo kimshikilia kwa miaka 43.
Ni chini ya maeneo bunge 10 kati ya 210, ambayo yalikuwa yameangaza matokeo siku ya Alhamisi, na kuifanya kuwa mapema mno kubainisha mwelekeo wowote wa kitaifa. Matokeo katika kinyang’anyiro cha urais hayakutarajiwa kwa siku nyingine au mbili, ingawa muda uliowekwa rasmi, kutangaza matokeo hayo ni siku tano.
Huku hayo yakiarifiwa, polisi walisema wamewakamata watu 41 na kukamata simu za mkononi, talakilishi na vifaa vingine vya kielektroniki wakati wa msako mkali katika maeneo manne mjini Harare kufuatia taarifa kuhusu “uasi na uhalifu”.