Gazeti la Daily Telegraph linadai Mbelgiji huyo ameamua hataki tena kujiunga na Juventus.
Ni hatua ya kushtua kutoka kwa Lukaku, ambaye hamu yake ya kujiunga na wababe hao wa Turin msimu huu wa joto ndiyo iliyowakasirisha Inter Milan na kumaliza harakati zao za kutaka kumsajili tena mshambulizi huyo wa kudumu kufuatia kurejea kwa mkopo San Siro msimu uliopita.
Lakini kucheleweshwa kwa mazungumzo na Juventus kumemfanya Lukaku kutafuta uhamisho wa mkopo kwenda Roma badala yake.
Awali Lukaku alikuwa amesisitiza kwamba angefikiria tu kuondoka Chelsea kwa kudumu msimu huu wa joto, lakini mabadiliko ya moyo yameifanya The Blues kubadili mipango yao pia, huku timu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza sasa ikifanya mazungumzo na Roma kuhusu mkataba.
Inasemekana Lukaku alikataa ofa kutoka Saudi Arabia msimu huu wa joto huku akitafuta kuendelea kushindana katika kiwango cha juu barani Ulaya.
Lakini ameweka wazi kuwa haoni mustakabali wake akiwa Chelsea, ambako amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21 na hata hajazungumza na Mauricio Pochettino kuhusu hali yake.