Meli ya Kwanza kubwa aina ya MV Innovation Way yenye urefu wa mita 250 kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), iliyobeba mitambo kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima, Uganda imewasili katika Bandari ya Tanga.
Meli hiyo imebeba mitambo mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa gati kubwa la Meli za mafuta litakalojengwa eneo la Chongoleani Jijini Tanga ikiwa ni sehemu ya mradi huo.