Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Jokate Mwegelo amewataka Wananchi Wilayani humo kutunza mazingira kwa kuacha kutumia mifuko ya Plastic na badala yake kutumia bidhaa zinazo tengenezwa na zao la Mkonge .
Jokate ameyasema hayo wakati akifungua jengo la Ofisi ya Chama cha ushirika cha wakulima wa zao la mkonge (MAGOMA AMCOS ) na kusema kuwa ni wakati wa jamii kuanza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuacha kutumia mifuko ya plastic na kutumia vifungashio vinavyo tengenezwa na zao la mkonge ili kutunza mazingira.
“Matumizi ya mifuko na kamba za Plastic zinapelekea uharibifu wa mzaingira,na suala la mazingira ni suala ambalo halina mbadala, Ili kukabiliana na uharibifu wa Mazingira mbadala wake ni kutumia bidhaa zinazotikana na zao la Mkonge. Niwaombe ndugu zangu na ninyi mkawe mabalozi wa kukataa matumizi ya mifuko ya plastic na kamba za Plastic.”
Aidha ameupongeza Uongozi wa Magoma AMCOS kwa KUJENGA Jengo lenye thamani zaidi ya shilingi Milioni Sabini na Mbili (72,000,000/=)na kuwa mfano wa kuigwa Tanzania kwa kuwa na Jengo zuri la chama Cha ushirika hasa kwenye zao la Mkonge.
Akisoma taarifa Meneja wa ushirika huo Maneno Jackson amesema Fedha hizo za kujenga Jengo hilo zimetokana na michango na tozo za wanachama wenyewe,huku akisema kupatikana kwa ofisi hiyo itawaongezea ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.