Shirika lisilo la kiserikali Wold Vision Tanzania wamefunga mradi wa Ruvu remit ambao umedumu takribani miaka 25 huko wilayani simanjiro Mkoani Arusha ambao umefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo kilimo,Ufugaji,Elimu,uchumi,maji,afya usafi wa mazingira pamoja na utetezi na Ulinzi wa watoto .
Subiria Mwanamo ambaye ni Mkurugenzi wa rasilimali watu kutoka Shirika hilo amesema kuwa wapo tayari kushirikiana na wanajamii wa ruvu remiti kutoa ushauri katika miradi mbalimbali ya maendeleo japo kwa sasa wamehitimisha mradi wao ndani ya Ruvu remit.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Simanjiro Mhe. Suleiman Serera ameeleza kuwa watahakikisha wanailinda miradi iliyofanyika ndani ya miaka 25 na kuzidi kuongeza miradi mingine na kufanya maboresho mbalimbali kama Serikali.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Abdallah Mwaipaya amesema watahakikisha miradi yote inalidwa na pamoja na kuiendeleza.