Maelfu ya watu walikusanyika wikendi hii mbele ya Lincoln Memorial huko Washington kuadhimisha maandamano ya Martin Luther King mwaka 1963 na hotuba yake maarufu. Maadhimisho, au muendelezo wa mapambano, wanabainisha waandaaji, ambao wanahofia kupungua kwa haki za watu weusi, hasa katika suala la ghasia za polisi.
Jamii ya Wamarekani weusi nchini Marekani wanalalamikia haki zao kuheshimishwa, wakibaini kwamba wanalengwa na vurugu za polisi kila mwaka.
Miaka 60 baada ya “ndoto” ya Martin Luther King, Joshua anatembea kati ya umati kwenye Makumbusho ya Lincoln huko Washington, na bango lenye picha za watu weusi waliouawa na polisi.
Mengi ya majina haya ni maarufu nchini Marekani hivi leo: George Floyd, Eric Gardner au hata Michael Brown, lakini wengine si maarufu sana, kama lile la mjomba wake, ambaye pia aliuawa na polisi. Kwa mujibu wa Joshua, 44, ukatili huu wa polisi unathibitisha kuwa pambano la Martin Luther King bado halijaisha:
“Pambano linaendelea na ninahisi kama mfumo haujabadilika sana. Kwa sababu, iwe umeuawa kwa kamba au kuuawa kwa risasi za polisi, kwa vyovyote vile, umekufa. ”
Vurugu za polisi ziko akilini mwa kila mtu hapa. Hivi karibuni au baadaye, kila mzazi mwenye asili ya Kiafrika lazima awe na majadiliano haya na watoto wao kuhusu polisi. Inaitwa “The Talk” katika jamii, amesema Gary kutoka New York.
Kwa wastani, polisi wa Marekani huua watu elfu moja kila mwaka, hatari kubwa maradufu kwa watu weusi.