Mahakama nchini Pakistan Jumatatu ilitupilia mbali kesi ya uchochezi dhidi ya Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan, wakili wake alisema kwenye jukwaa la ujumbe X, ambalo zamani lilijulikana kama Twitter, Jumatatu.
“Mungu apewe sifa,” wakili wake Naeem Panjutha aliandika kwenye X, zamani Twitter, siku ya Jumatatu.
Panjutha alisema kuwa mashtaka hayo, ambayo yalihusiana na mauaji ya wakili katika mji wa kusini wa Quetta, yametupiliwa mbali na Mahakama Kuu ya Balochistan.
Bw Khan alishtakiwa kwa mauaji hayo mwezi Juni mwaka huu, na amekuwa akikabiliana na hili na karibu kesi nyingine 170 zilizoletwa dhidi yake tangu alipotimuliwa ofisini. Amekana mashtaka hayo, ambayo ni ya ufisadi hadi uchochezi, kama yalivyochochewa kisiasa.
Alikamatwa mapema mwezi huu kuhusiana na kesi ya ufisadi na anaendelea kuzuiliwa.
Mapema mwezi huu, mahakama ya kesi ilimpata Bw Khan na hatia ya kuuza zawadi za serikali kinyume cha sheria, inayojulikana kama kesi ya Toshakhana, na kumhukumu kifungo cha miaka mitatu jela.
Kesi tofauti pia ilikuwa ikifanyika Jumatatu katika Mahakama Kuu ya Islamabad ambapo mawakili wa Bw Khan walikuwa wakikata rufaa ili hukumu hiyo isitishwe.
Bw Khan anasalia katika gereza lenye ulinzi mkali la Attock kuhusiana na kesi ya ufisadi.
Khan alikamatwa mara baada ya hukumu ya mahakama katika mji wa mashariki wa Lahore.