“Baada ya Taliban kufunga vyuo vikuu vya wanawake, tumaini langu pekee lilikuwa kupata ufadhili wa masomo ambao ungenisaidia kusoma nje ya nchi,” anasema mwanafunzi wa Afghanistan mwenye umri wa miaka 20 Natkai.
Jina la Natkai limebadilishwa kwa usalama wake mwenyewe.
Taliban wamewakandamiza vikali wanawake wanaowapinga.
Natkai anasema aliendelea kusoma ingawa kulikuwa na nafasi ndogo ya yeye kuhudhuria chuo kikuu katika nchi yake.
Kisha akapewa ufadhili wa kusoma katika Chuo Kikuu cha Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kutoka kwa mfanyabiashara bilionea wa Imarati Sheikh Khalaf Ahmad Al Habtoor.
Ufadhili wa masomo kwa wanawake wa Afghanistan ulitangazwa mnamo Desemba 2022 baada ya Taliban kupiga marufuku wanawake kutoka chuo kikuu.
Shirika la habari la BBC limeripoti kuwa kuwa jumla ya wanawake 100 wa Afghanistan wamefaulu kupata ufadhili huu.
Baadhi ya wanafunzi wa Afghanistan wanaoishi nje ya nchi tayari wamesafiri hadi Dubai.