Shirikisho la Soka la Saudi Arabia (SAFF) limesema Muitaliano huyo amepewa kandarasi ya miaka minne. Mechi zake za kwanza kufundisha zitakuwa dhidi ya Costa Rica Septemba 8 na Korea Kusini siku nne baadaye – zote ni za kirafiki na zitafanyika Newcastle.
Roberto Mancini aliteuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Saudi Arabia Jumapili, wiki mbili tu baada ya meneja huyo aliyeshinda Ubingwa wa Ulaya kuacha kazi yake ya kuinoa Italia.
Shirikisho la Soka la Saudi Arabia (SAFF) limesema Muitaliano huyo amepewa kandarasi ya miaka minne. Mechi zake za kwanza kufundisha zitakuwa dhidi ya Costa Rica Septemba 8 na Korea Kusini siku nne baadaye – zote ni za kirafiki na zitafanyika Newcastle.
SAFF ilichapisha video kwenye mitandao ya kijamii ikiwa na sehemu za Mancini. Ndani yake, anasema: “Niliweka historia Ulaya, sasa ni wakati wa kuweka historia na Saudi.”
Vyombo vya habari vya Italia viliripoti kwamba kandarasi ya Mancini ina thamani ya euro milioni 25 (dola milioni 27) kwa mwaka na kwamba mwenye umri wa miaka 58 atawasilishwa kwa vyombo vya habari katika mkutano wa wanahabari siku ya Jumatatu.
Mancini ndiye jina kubwa la hivi punde kuwa sehemu ya mapinduzi ya soka ya Saudia.
Vilabu kutoka nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta vilimwaga pesa hizo katika msimu wa kiangazi kwa wachezaji kadhaa nyota huku kukiwa na wasiwasi unaoendelea kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu ambayo yanahoji kuwa Saudi Arabia inatumia michezo kwa madhumuni ya mahusiano ya umma.