Wananchi wa kimara mavurunza Mtaa wa Milenia ya tatu shina namba saba, wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya barabara ya mtaa wao kutopitika kutokana na ubovu wa barabara hiyo hali inayopelekea kushindwa kupata huduma za kijamii kwa uharaka haswa wakati wa mvua,
Changamoto hiyo imepelekea wananchi hao kujichangisha kiasi cha pesa na kutengeneza barabara hiyo ya mtaa wao kwa kiwango cha zege, Ambapo mpaka sasa wameweza kutumia milioni 25 ili kuweza kukamilisha zoezi la umwagaji zege katika barabara hiyo
Akizungumza na waandishi wa habari Mjumbe wa mtaa huo Asha mwakipesile amesema Barbara hiyo ina urefu wa mita 1200 ambapo mpaka sasa wameweza kumwaga zege mita 800 tu , Huku mita zilizobaki ni 400 ambazo ndio zinawapa ugumu wakumaliza mladi huo,
kutokana na ugumu wa kipande kilichobaki wameomba msaada wa serikali katika kuwasaidia kufanikisha umalizaji wa mita 400 zilizobaki kwani Barabara hiyo ndio inayotumika na wakazi wa eneo ilo na kuwawezesha kuzifikia huduma za jamii kwa uharaka zaidi