Wenyeji katika kijiji hicho cha Austria cha Hallstatt wamefanya maandamano dhidi ya utalii mkubwa kwa kuziba barabara kuu ya kuelekea mjini kwa kudai kuwa kina idadi ya watu 800 tu, lakini hupata hadi wageni 10,000 kwa siku wakati wa msimu wa juu wa watalii.
Wakazi wanatoa wito wa kuweka mipaka kwa idadi ya watalii wa kila siku, na kupiga marufuku mabasi ya watalii baada ya 17:00 saa za ndani.
Ingawa utalii umekuwa mzuri kwa uchumi wa Hallstatt, baadhi ya wenyeji wanasema kuna wageni wengi sana.
Hallstatt, pamoja na nyumba zake za kupendeza za zamani kwenye ufuo wa ziwa safi la Alpine lililozingirwa na milima , imekuwa sehemu kubwa ya utalii katika miaka ya hivi karibuni.
Mnamo 2006, iliangaziwa katika tamthilia ya kimapenzi ya Korea Kusini – ikikuza umaarufu wake huko Asia – ikiwa na mfano wa mji huo uliojengwa nchini Uchina miaka sita baadaye.
Wageni wengi huja kutafuta picha nzuri ya kujipiga wenyewe, pamoja na ziwa, mnara wa kanisa mwembamba wa rangi ya kijivu na mandhari nzuri ya mlima .
Kama mojawapo ya maeneo yenye watalii wengi zaidi barani Ulaya baadhi ya wenyeji wanasema kuna wageni wengi sana, hasa wasafiri wa mchana, ambao husafirishwa kwenda mjini kwa makochi makubwa.