Katika Maendeleo ya Kilimo Cha Mkonge nchini Tanzania inaelezwa kuwa zao la mkonge liliingizwa nchini Tanganyika mwaka 1892 na mtaalamu wa kijerumani Dkt. Richard Hindorff, ambaye alikuwa ni mtafiti wa mimea na udongo.
Mtaalamu huyo alichukua miche 1000 kutoka Pwani ya Mexico kwenye jimbo la Yuctan na kuisafirisha kupitia Frolida, Marekani na Humburg, Ujerumani.
Kati ya miche 1000, ni miche 62 tu ndiyo iliyofika Tanganyika na ilipandwa sehemu iitwayo Kikokwe huko Pangani, Tanga.
Uzalishaji wa mkonge nchini Tanzania ulianza mwishoni mwa karne ya 19 na ulisimamiwa na Kampuni ya Serikali ya Kikoloni ya Kijerumani iliyoitwa German East Africa.
Wakati wa Uhuru mwaka 1961, Tanzania ilikuwa muuzaji mkuu wa mkonge Duniani na Sekta hiyo iliajiri Wakulima na wafanyakazi wa viwandani zaidi ya milioni 1