Akiwa madarakani kwa miaka 14, rais wa Gabon Ali Bongo Odimba amechaguliwa tena katika uchaguzi wa Jumamosi kwa asilimia 64.27 ya kura zilizopigwa, mamlaka ya kitaifa inayosimamia uchaguzi huo imetangaza leo Jumatano. Mpinzani wake mkuu Albert Ondo Ossa amepata asilimia 30.77 pekee ya kura.
Kituo cha Uchaguzi cha Gabon kimetangaza Jumatano kuchaguliwa tena kwa rais Ali Bongo kwa 64.27% ya kura dhidi ya 30.77% ya mpinzani wake mkuu Albert Ondo Ossa, ambaye ameshutumu “udanganyifu uliopangwa na kambi ya Bongo” saa mbili kabla ya uchaguzi siku ya Jumamosi.
Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba, aliye madarakani kwa miaka 14, alishinda muhula wa tatu katika uchaguzi wa Jumamosi kwa asilimia 64.27 ya kura zilizopigwa, mamlaka ya kitaifa ya upigaji kura ilitangaza Jumatano (tarehe 30 Agosti).
Ali Bongo alimshinda, katika kura moja ya raundi, mpinzani wake mkuu Albert Ondo Ossa, ambaye amepata asilimia 30.77 pekee ya kura, pamoja na wagombea wengine 12 waliokusanya makombo tu, Rais wa Kituo cha Uchaguzi cha Gabon (CGE), Michel. Stéphane Bonda, ametangaza kwenye televisheni ya serikali ya Gabon 1ère.
“Baada ya kukusaywa kwa matokeo (…) amechaguliwa Bongo Ondimba Ali kwa kura 293,919 sawa na 64.27%”, ametangaza Stéphane Bonda. Kiwango cha ushiriki kilikuwa 56.65%.