Mamia ya wanajeshi wa Gabon, kupitia taarifa kwenye televisheni ya kitaifa, wametangaza kumaliza utawala wa sasa pamoja na kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi yaliompa ushindi rais Ali Bongo Ondimba.
Wakati wa tangazo hilo, wanahabari wameripoti kusikika kwa milio ya risasi katika mji mkuu wa Gabon, Libreville.
Wakitangaza hatua hiyo ya kufuta matokeo ya uchaguzi huo, wanajeshi hao wamesema taasisi zote za serikali pia zimevunjwa.
Mmoja wa wanajeshi hao amesema wamechukua hatua ya kumaliza utawala wa sasa kama njia moja ya kulinda amani ya nchi hiyo.
Taarifa hiyo pia ilitangazwa kwenye televisheni ya kitaifa ya Gabon.
Tukio hilo limekuja muda mfupi baada ya tume ya uchaguzi nchini humo kumtangaza Gabon mshindi wa uchaguzi huo.
Bongo ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 14, alikuwa ameshinda uchaguzi kwa awamu ya tatu kwa kupata asilimia 64.27 ya kura.
Mpîzani mkuu wa Bongo, Albert Ondo Ossa, alipata asilimia 30.77 ya kura hizo kwa mujibu wa matokeo.