Wachezaji wanne wa Arsenal walijumuishwa kwenye kikosi bora cha mwaka cha PFA cha mwaka huu.
Nao ni: Bukayo Saka, Aaron Ramsdale, Martin Odegaard na William Saliba.
Saka aliunganishwa katika mashambulizi na Erling Haaland wa Manchester City na nyota wa zamani wa Tottenham, Harry Kane.
Wachezaji wenzake wa Haaland Rodri na Kevin de Bruyne wamechaguliwa katika safu ya kiungo, huku John Stones na Ruben Dias wakiwa katika ulinzi.
City ilimaliza kwa pointi tano mbele ya Arsenal msimu uliopita na kushinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza.
Timu Bora ya Mwaka hupigiwa kura na wachezaji wenzao wa kulipwa.
Beki wa Newcastle United, Kieran Trippier, alichaguliwa kuwa beki wa kulia.
Chelsea, Manchester United na Liverpool hawakuwa na wachezaji waliojumuishwa.