Mtoto mchanga ameokolewa kutoka kwenye choo cha shimo huko Otuocha, Eneo la Serikali ya Mitaa ya Anambra Mashariki siku tatu baada ya kuzaliwa.
Kulingana na ripoti iliyotumwa kwenye ukurasa wa Facebook wa wizara ya wanawake na ustawi wa jamii ya jimbo la Anambra, tukio hilo lilitokea Jumapili.
Mama wa mtoto huyo wa kiume, Nwaedoka Chidinma, msichana mwenye umri wa miaka 20 kutoka Izzi, Jimbo la Ebonyi, alisemekana kutekeleza kitendo hicho kimakusudi.
Esther Omesi, mkulima na rafiki wa Chidinma, alitahadharisha mamlaka husika kuhusu tukio hilo.
Alisimulia kuwa Chidimma alichukua muda chooni na alipotoka nje, damu zilichuruzika hali iliyomfanya amuite nesi aliyemkagua na kubaini kuwa mtoto hayupo.
Akifichua zaidi jinsi ilivyokuwa, Omesi alisema kwamba walisikia kilio cha mtoto Jumanne asubuhi na haraka walitumia ngazi kumuokoa mtoto huyo.