Msanii wa BongoFlava Haitham Kim amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Temeke kufuatia kuugua kwa Muda wa wiki Sasa tatizo likisemwa kuwa ni changamoto ya Upumuaji, taarifa za kuugua Kwa msanii Haitham Kim zimethibitishwa na Mume wake Bryaison maarufu kama Bosheni.
Bosheni amedai kuwa Haitham amepatwa matatizo ya kupumua na kuwekwa ICU ambapo anatumia mashine kumsaidia kupumua huku akichoma sindano za laki 7 Kwa siku na leo inakua siku ya Tatu kitu ambacho Kimewazidia Familia hivyo kuomba msaada Kwa wadau na Mashabiki zake kuweza kumchangia ili aweze kupatiwa matibabu na kurudi katika hali yake.