Serikali imesema imejipanga kuja na program za kimkakati zitakazojikita kwenye masuala ya Watoto wa kiume kwa kuwapeleka jando la kisasa ambalo litawasaidia kupata miongozo inayoelekeza maana ya kuwa baba ili wanapokuwa wakubwa wajue changamoto watakazokutana nazo kwenye ndoa.
Hayo yamesemwa Bungeni jijini Dodoma leo Agost 31,2023 na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalum, Dkt Dorothy Gwajima wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Hai, Saashisha Mafue aliyetaka kujua mpango wa serikali katika kumsaidia mtoto wa kiume ili awe kiongozi mzuri wa familia.
Dkt Gwajima amesema mpango huo wa kuwawezesha na kuwaendeleza vijana balehe kuanzia miaka 10 hadi 19 utajikita katika kuongeza nguvu katika uwekezaji kwa kuja na mkakati huo kwani zamani walipelekwa jando lakini sasa watapelekwa jando la kisasa.
tazama zaidi……