Polisi nchini Uganda wana wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa idadi ya watoto wachanga na watoto wadogo wanaotelekezwa katika mji mkuu wa Kampala.
Wanasema angalau vijana 30 walio chini ya umri wa miaka 8 hutupwa mjini kila mwezi.
Uhalifu wa kuwatelekeza watoto umeweka mzigo wa ziada kwa nyumba za kulelea watoto ambao hutegemea hisani. Hii hapa ripoti…
Polisi ya Uganda inasema inapokea simu zaidi na zaidi kutoka kwa watu wanaopata watoto wachanga waliotelekezwa mjini humo.
Watoto hao wengi huachwa kwenye sehemu za kutupia taka na kando ya barabara anasema Patrick Onyango, msemaji wa polisi, mji mkuu wa Kampala.
“Katika kituo hiki cha polisi cha kati mjini Kampala mwezi wa Agosti tuliandikisha watoto wawili walioachwa au kutelekezwa…na hicho ni kituo kimoja tu cha kusajili kesi mbili na tuna vituo kumi na tisa ukijumlisha vyote vitaongeza idadi”
Kulingana na ripoti ya uhalifu ya Polisi ya 2022 taasisi hiyo ilirekodi ongezeko la asilimia 23 ya uhalifu wa kutoroka kwa watoto.
Mamlaka za mitaa zinalaumu uhalifu wa kuwatelekeza watoto kwa akina baba kuwanyima ubaba, mimba zisizotarajiwa na wazazi kuhangaika kumudu kuwatunza.
Na baada ya kushindwa kuwatafuta wazazi wao, polisi huwaweka watoto katika nyumba za kulea watoto.
Lakini nyingi ya taasisi hizi za kulelea watoto zimejaa kupita kiasi.
“Sasa hivi ninakazwa, unaona bega linakaza kwa sababu siwezi kuwamudu…tunajaribu kuona kwamba wakikua na kufikia umri ambao wanaweza kujisimamia lazima tuwaachie. “