Mfalme wa Thailand amebadilisha kifungo cha miaka minane jela cha Waziri Mkuu wa zamani Thaksin Shinawatra hadi mwaka mmoja, siku moja baada ya bilionea huyo kuwasilisha ombi la msamaha.
Msamaha huo wa sehemu kutoka kwa Mfalme Maha Vajiralongkorn ulithibitishwa na Gazeti rasmi la Royal Gazette na tangazo lililoashiria utumishi wake kwa nchi kama waziri mkuu.
“Thaksin alikubali uhalifu wake na alionyesha majuto,” gazeti la serikali lilisema Ijumaa.
Alifika kwa ndege ya kibinafsi wiki iliyopita na kuhamishiwa gerezani kutumikia kifungo cha miaka minane. Usiku wake wa kwanza, alihamishwa hadi hospitali ya polisi kwa sababu ya maumivu ya kifua na shinikizo la damu.
Kiongozi huyo wa zamani, mwenye umri wa miaka 74, alirejea Thailand katika hali ya kustaajabisha baada ya kukaa miaka 15 nje ya nchi katika uhamisho wake binafsi ili kuepuka jela kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na migongano ya kimaslahi wakati alipokuwa madarakani.
Thaksin “alikuwa waziri mkuu, amefanya mema kwa nchi na watu, na ni mwaminifu kwa ufalme”, gazeti la serikali lilisema.
“Aliheshimu mchakato, alikubali hatia yake, alitubu, akakubali maamuzi ya mahakama. Hivi sasa yeye ni mzee, ana ugonjwa unaohitaji huduma kutoka kwa mtaalamu wa matibabu,” ilisoma.
“Mfalme wake Mfalme amempa msamaha na kupunguza adhabu kwa Thaksin Shinawatra … ili aweze kutumia ujuzi na uzoefu wake kuendeleza nchi zaidi.”
Thaksin alichaguliwa kuwa waziri mkuu mara mbili na kuondolewa katika mapinduzi ya kijeshi ya 2006