Kutoka msibani Tabata Kimanga nyumbani kwa Mume wake Haitham watu mbalimbali wameendelea kufika kuombelezea wakingojea taratibu nyingine ambazo ni mazishi yanayotarajiwa kufanyika saa 10 jioni katika makaburi ya Kisutu.
@AyoTV_ imeongea na Msemaji wa Familia upande wa Mume wa Marehemu, BenQ Johnson ambaye ametoa taratibu zote za mazishi na kuelezea mchango uliotolewa na Wasanii wa Bongo Fleva kuanzia wakati wa matibabu na hata mazishi ambapo amesema kuwa “Niliwasiliana na Brother Sogydogy kuna michango ya Wasanii kama Chama chao walituma”
“Mara ya kwanza michango ilitoka sababu ya matibabu lakini michango niliyopokea Mimi leo wametusaidia kama kwenye usafiri na mambo mengine, mara ya kwanza Soggy aliniambia walimtumia Boshen (Mume wa Haitham) laki 4, mara ya pili laki 5”