Baada ya miezi kadhaa ya ukame wa kihistoria, Uhispania inakumbwa na mvua kubwa iliyosababisha vifo vya watu watatu na watatu hawajulikani waliko, huku mtoto wa miaka kumi akinusurika kuzama baada ya kukimbilia kwenye mti.
Mvua hizi, ambazo zimekuwa zikiathiri nchi tangu mwishoni mwa wiki hii, zimeathiri hasa mikoa ya Madrid na Castile-La Mancha, katikati mwa Uhispani, ambako mvua ilinyesha usiku wa siku ya Jumapili kuamkia Jumatatu.
Rais wa Castile-La Mancha, Emiliano García-Page, alitangaza Jumatatu asubuhi kwenye mitandao ya kijamii “vifo vya watu wawili katika jimbo la Toledo”, katika maeneo ya Casarrubios del Monte na Bargas. Hakutoa maelezo kuhusiana na mazingira ya vifo hivyo.
Walinzi wa Kiraia walitangaza baadaye mchana kifo cha mtu wa tatu, mtu wa miaka 50 ambaye mwili wake ulikuwa karibu na mkondo huko Camarena, katika mkoa huo wa Toledo.
Utafutaji pia unaendelea ili kupata, katika eneo hilo, “mwanamke aliyetoweka kufuatia mafuriko (ya mto) huko Valmojado”, pia kikosi cha walinzi wa raia kimebainisha.