Beki wa kimataifa wa Panama Gilberto Hernandez ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa na umri wa miaka 26,ligi ya soka ya Panama ilithibitisha habari hiyo katika taarifa.
Kisa hicho kilitokea katika mji wa Colon lakini haijafahamika iwapo Hernandez ndiye aliyelengwa na shambulizi hilo,wengine saba walijeruhiwa katika tukio hilo.
Hernandez aliichezea nchi yake mara mbili na mechi moja ilikuja katika kupoteza kwa 2-0 dhidi ya Argentina, ambapo Lionel Messi alifunga, Machi mwaka huu.
Huo ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Argentina mbele ya mashabiki wa nyumbani tangu washinde Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka jana.
Baba wa mchezaji huyo amewataka vijana wa Colon ‘kuacha vurugu’ na kutoa wito kwa mamlaka ‘kuanzisha miradi ya kuokoa vijana na vurugu hizi’.
Pia alinukuliwa na BBC akiwataka wauaji wa mtoto wake kujisalimisha. Kwa mujibu wa The Guardian, kuna mtu mmoja aliyekamatwa hadi sasa na polisi.
Shirikisho la Panama pia lilitoa taarifa, likisema linajutia kifo cha kusikitisha cha Gilberto Hernandez