Liverpool wanaripotiwa kujiandaa kwa dau kubwa la pauni milioni 215 kutoka kwa Al Ittihad kumnunua nyota Mohamed Salah.
Wiki iliyopita, iliripotiwa sana kwamba klabu ya Ligi ya Soka ya Saudia Al Ittihad ilikuwa na nia ya kutaka kumsajili Salah kutoka Liverpool.
Iliripotiwa kuwa Liverpool ilikataa dau la pauni milioni 150 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 baada ya Jurgen Klopp kusema hadharani kwamba Salah hauzwi.
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Al Ittihad wanatazamiwa kuwajaribu tena Liverpool kwa dau nono la pauni milioni 215.
Ripoti hiyo ilidai kuwa dau hilo litakuwa la pauni milioni 170 pamoja na nyongeza.
Inaaminika kuwa Salah atapewa ofa ya pauni milioni 2.45 kwa wiki ili kuondoka Liverpool.
Mbali na mishahara hiyo kubwa, Salah pia amepewa asilimia kubwa ya mauzo ya shati, bonasi ya kushinda ya Pauni 55,000 pamoja na majukumu ya ubalozi kwa kampuni tatu kubwa za Saudi.
Imesemekana kwamba kila kampuni itakuwa tayari kumlipa pauni milioni 6, ambayo ina maana kwamba Salah atachukua pauni milioni 18 zaidi juu ya mkataba wake mkubwa.