Zaidi ya wajumbe 4,000 kutoka zaidi ya nchi 70 wanakutana kwenye Kongamano la 13 la kila mwaka la Mifumo ya Chakula Afrika, kujadili mabadiliko ya mifumo ya chakula barani Afrika.
Mkutano huo wa siku nne, utalenga zaidi kujadili mabadiliko ya mifumo ya chakula na kuhakikisha uhakika wa chakula kwa wote.
Taarifa iliyotolewa na waandaaji wa kongamano hilo imesema kongamano hilo linafanyika Septemba 5-8 likiwa na kauli mbiu ya “Rejesha, Unda upya, Chukua hatua: Suluhu za Afrika kwa Mabadiliko ya Mifumo ya Chakula,” linawakutanisha viongozi, na wavumbuzi kutoka kote duniani kujadili sera, mafanikio na uvumbuzi katika mabadiliko ya mifumo ya kilimo na chakula.
Rais Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza na kujadili na viongozi wa mataifa mbalimbali, wataalamu, wawekezaji, vijana na wengineo juu ya namna Afrika inaweza kuendeleza na kuja na njia mbadala ili kunufaika na kilimo cha chakul
Waziri wa Kilimo wa Mh. Hussein Bashe amesema kongamano hilo ni hatua muhimu katika safari ya kuanzisha mageuzi ya mifumo jumuishi na endelevu ya chakula katika bara zima la Afrika.