Habari ya Asubuhi..! karibu kwenye matangazo yetu mubashara hii leo….
Tanzania inatajwa kuwa chanzo cha baraka kufuatia amani, utulivu na rasilimali za nchi kutokana na uwepo wa uongozi unaozingatia haki.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mchungaji kiongozi wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, Baba Halisi alisema inatakiwa Watanzania kujua jinsi nchi ya Tanzania ilivyobarikiwa na Mwenyezi Mungu kwa kuwa rasilimali za kutosha.
Halisi alisema inatakiwa Watanzania wajitambue na kubadilisha mienendo yao kwa kuhakikisha wanakuwa baraka kwa wengine.
“Kwa kuwa Tanzania imebarikiwa, Watanzania wanapaswa kubadilisha mienendo yao kwa kuchangua namna bora ya kuishi ili kuendelea kuwa baraka kwa mataifa mengine,” alisema
Halisi alisema kanisa hilo limekuwa likiishi kwa kuhimiza amani, upendo, kuzalisha haki ndio maana limeandaa mkutano wa kijamii utakaofanyika Septemba 10, jijini Dar es Salaam na zaidi ya watu 1000 kutoka ndani na nje ya nchi watashiriki.
Alisema mkutano huo utabebwa na mada isemayo Tanzania ndiyo chanzo cha baraka kwa mataifa yote lengo ni kuwapa uelewa Watanzania kuzitambua rasilimali zilizopo.
“Kanisa hili ili kuhakikisha rasilimali zinalindwa ikiwepo amani, upendo na kuzalisha haki, tumekuwa na desturi ya kila siku saa 11 asubuhi kuwaombea viongozi waliopo madarakani wazidi kuongoza kwa haki,”alisema.