Huyu ni Michael Charles (34) Baba wa watoto watatu, makazi yake ni Bunda mkoa wa Mara, ni miaka minne kijana Michael yupo kitandani baada ya kupata ajali ya gari akiwa njiani kuelekea Mwanza mwaka 2019.
October 25, 2019 ni kumbukumbu yenye maumivu kwa kijana huyu kwani ndiyo siku aliyopata ajali na kupelekea kuvunjika pingili ya shingo na uti wa mgongo kwa mujibu wa Madaktari.
Leo hii Michael hana tena uwezo wa kutembea kwa miguu yake, wala kula kwa mikono yake na hata haja hutumia mpira, kitu kina muumiza Michael ni kuwa miezi miwili mara baada ya kupata ajali mke wake aliondoka kwa kushindwa kuvumilia hali ya mume wake licha ya kuwa walipata watoto.
Familia ya kijana huyu umeuza kila kitu ili tu ndugu yao arejee kwenye hali yake ila pesa bado haijatosha, Michael anasema kinahitajika kiasi cha zaidi ya milioni Tsh. 20, ili afanyiwe upasuaji wa nyonga na huwenda ikarejerea kawaida.
Ili kuitazama kwa urefu stori ya hii ya MICHAEL nenda YouTube ‘millardayo’
Namba ya kumpata Michael Charles 0758 106 730.