Waziri wa Ulinzi wa Russia ameashiria mashambulio ya kigaidi yaliyofanywa na Ukraine dhidi ya maeneo ya raia nchini humo na kutoa takwimu za vifo na hasara za uharibifu ilizopata Kiev katika operesheni ilizotekeleza kujibu mashambulio ya Moscow.
Sergei Shoigu alitoa takwimu hizo jana Jumanne alipohutubia hadhara ya makamanda wa kijeshi wa nchi hiyo na kutangaza kwamba jeshi la Ukraine limepoteza wanajeshi 66,000 na silaha 7,600 tangu lilipoanzisha operesheni za kujibu mapigo ya mashambulio ya Russia.
Shoigu ameendelea kueleza kwamba licha ya kupata hasara kubwa, serikali ya Ukraine inajaribu kuendelea na operesheni zake za kujibu mashambulio ya Russia.
Waziri wa Ulinzi wa Russia ameongeza kuwa, vikosi vya jeshi la nchi hiyo vimeteketeza makombora 159 aina ya Hymars, zaidi ya ndege elfu moja zisizo na rubani na makombora elfu kumi na tatu aina ya cruise katika operesheni za kijeshi ilizotekelezea ndani ya ardhi ya Ukraine katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita