Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF,Jijini Dar es salaam leo ambapo amesema programu ya kuwajengea kesho bora Vijana (BBT) inalenga kutengeneza ajira rasmi milioni 3 ifikapo 2030 na itapelekea kuanzishwa kwa biashara za Vijana 12,000 zenye faida.
“Kama Mwenyeji wenu, mniruhusu nisimulie hadithi kuhusiana na programu ya kilimo kwa vijana nchini Tanzania, Nchi hii ilianzisha ajenda ya kufanya kilimo kuchangia kwa 10% kwenye Pato la Taifa ifikapo mwaka 2030 ili kutekeleza ajenda hiyo tuliunda programu inayoitwa Kujenga Kesho Bora kwa Vijana wa Tanzania (BBT) lengo likuwa ni kuimarisha ushiriki wa Vijana katika Sekta ya Kilimo na kuboresha maisha huku wakichangia juhudi za sasa za kupunguza ukosefu wa ajira.
“Lengo la kimkakati la BBT ni kuhamasisha Vijana kushiriki katika miradi endelevu kupitia uzalishaji wa mazao, ufugaji na uvuvi, kuwawezesha Vijana kupitia mafunzo na ushauri, kushirikisha Vijana katika usimamizi wenye faida wa kilimo biashara na kuziwesesha biashara zinazoongozwa na Vijana kwa kuboresha mazingira ya biashara”
“Mpango huu unalenga kutengenezaji ajira milioni 3 rasmi ifikapo 2030 na kwa kuongeza katika kipindi hicho BBT inatarajiwa kusababisha kuanzishwa kwa biashara za Vijana 12,000 zenye faida, tangu kuanzishwa kwake mwaka 2022 BBT imefanikiwa kuajiri Vijana na Wanawake 1252 na hadi sasa 812 wameandikishwa kufanya mafunzo ya Kilimo Biashara ya miezi 4 katika Sekta 13 za incubation kwa mazao na 240 kwa mifugo 200 kwa uvuvi”