Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi amefurahishwa na Programu ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT) ambapo amesem programu hiyo ni moja ya suluhu za kutatua changamoto nchini.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo wakati akiongea na Wadau kwenye mkutano wa kuonesha fursa za uwekezaji kwenye programu ya kielelezo ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT) ambao umefanyika jijini Dar es Salaam Septemba 7, 2023.
Dkt. Mwinyi amesema mkutano huo umelenga kuonesha fursa kwa Wadau na kuwahamasisha kuunga mkono programu hiyo ya BBT.
Mkutano huo ni sehemu ya Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF) unaoendelea Jijini Dar es Salaam.