Kourtney Kardashian amewashukuru madaktari kwa “kuokoa maisha ya mtoto wake” kwa kumfanyia upasuaji mtoto wake ambaye bado hajazaliwa.
Nyota huyo 44, alisema alikimbizwa katika “upasuaji wa haraka wa fetasi”, ambapo madaktari wapasuaji huwafanyia watoto wachanga wakiwa bado tumboni.
“Kama mtu ambaye nimepata ujauzito mara tatu siku za nyuma, sikuwa tayari kwa hofu hiyo,” alisema.
Wanandoa hao hawajafichua aina ya upasuaji wa mtoto huyo wa kiume.
Katika ujumbe wake kwenye Instagram, Kourtney aliandika: “Nitawashukuru sana madaktari wangu wa ajabu kwa kuokoa maisha ya mtoto wetu.
“Ninamshukuru milele mume wangu ambaye alikimbia upande wangu kutoka kwenye ziara ili kuwa nami hospitalini na kunihudumia baadaye, mwamba wangu.
“Na kwa mama yangu, asante kwa kunishika mkono katika hili.”
Aliongeza: “Sidhani kama mtu yeyote ambaye hajapitia hali kama hiyo anaweza kuanza kuelewa hisia hiyo ya woga.
“Nina uelewa mpya na heshima kwa akina mama ambao wamelazimika kupigania watoto wao wakiwa wajawazito.
“Mungu asifiwe. Kutoka hospitalini nikiwa na mtoto wangu wa kiume tumboni mwangu na salama ilikuwa baraka ya kweli.”
Nyota huyo ana watoto watatu wenye umri wa miaka minane, 11 na 13 na Scott Disick.
Hapo awali alizungumza juu ya shida zake za kupata mimba na Barker, 47.
Lakini mnamo Juni alichapisha video ya Instagram ikimuonyesha akishikilia ishara kwenye tamasha la Blink-182 akisema: “Travis nina mimba.”