Ni Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi Mhe Goodluck Mlinga amekamata ng’ombe zaidi ya 1500 katika kata ya Mbaya baada ya kufanya doria wilayani humo mkoani Lindi Mnamo Septemba 5, 2023.
Mhe Goodluck Mlinga amekuwa akifanya doria katika kata mbalimbali Wilayani Liwale baada ya kuwa na Changamoto kubwa ya wafugaji kuvamia na kuingia kwenye hifadh, pia kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima kupelekea kufanya uharibifu wa mazao pia kuchangia wanyama pori hususani tembo kutoka kwenye hifadhi na kuingia lwenye makazi ya watu.
Kutokana na Uharibifu uliofanyika kwenye kata hiyo ikiwemo uharibifu wa mikorosho michanga na Uharibifu wa miundombinu ya maji kutoka kata ya mbaya kwenda kichonda, watatakiwa kulipa fidia kwa wakulima kwa uharibifu wa mazao, kulipa faini kwa Halmashauri na kuondoa mifugo yao kwa lori kuitoa mkoa wa Lindi kuirudisha ilipotoka.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka Viongozi wa Vijiji kutowapokea wafugaji ambao hawatambuliki na hawajasajiliwa kwenye vijiji husika na kama kijiji hakipo kwenye mpango wa ufugaji hakuna kupokea mfugaji.
Pia amewasisitiza kutoa taarifa mara moja pindi wafugaji watakapoingia kwenye maeneo ya kinyume na taratibu zilizopangwa ila kuzuia vitendo vya uharibifu wa mazao, miundombinu na mapigano kati ya Wakulima na Wafugaji.