Taasisi ya Benki ya CRDB Bank Foundation kupitia programu ya #IMBEJU na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ilala wameandaa maonesho ya wajasiriamali zaidi ya elfu tatu (3,000) kwa mwaka 2023, Wajasiriamali kutoka wilaya ya Ilala ambao ni wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 kutoka Halmashauri, na waalikwa wengine kutoka wilaya nyingine Dar es Salaam.
Lengo la Maonyesho hayo ni kutoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo kuonyesha bidhaa zao, kutengeneza mtandao wa biashara na kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara wengine pamoja na wataalam wa masuala ya biashara nchini.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari, Tully Esther Mwambapa, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, walisema, Maonesho hayo yatakuwa ya siku tatu kuanzia tarehe 11 hadi 13 Septemba katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na yataambatana na ugawaji wa vifaa pamoja na fedha taslimu milioni moja (1M) k