Idadi ya Watu waliofariki baada ya tetemeko la ardhi kutokea nchini Morocco imefikia zaidi ya Watu 2000 huku Watu wengine zaidi ya 2000 wakiwa wamejeruhiwa katika janga hilo.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco imesema tetemeko hilo kubwa lisilo la kawaida limesababisha uharibifu wa majengo katika Vijiji vya milima ya Atlas hadi kwenye Mji wa kihistoria, Marrakech.
“Watu 2012 wamefariki, wengine 2059 wamejeruhiwa huku Watu 1404 kati yao hali zao zikiwa mbaya, zoezi la kuwatoa Watu wengine waliofukiwa chini ya vifusi linaendelea”