Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limeeleza wasiwasi kutokana na kuongezeka kwa milipuko ya mabomu yaliyotegwa ardhini yaliyosababisha vifo vya watoto 30 tangu mwezi Juni mwaka huu nchini Somalia.
Kaimu mwakilishi wa UNICEF nchini Somalia Nejmudin Kedir Bilal amesema, hivi karibuni, watoto wengi wamekuwa wahanga katika matukio matatu tofauti yaliyohusika na kulipuka kwa mabomu hayo.
Katika taarifa yake aliyoitoa mjini Mogadishu, Bw. Bilal amesema watoto wanne wameripotiwa kuuawa, na wengine watano kujeruhiwa vibaya baada ya kucheza na mabaki ya silaha za kivita.
UNICEF imetoa wito kwa pande zote husika za mapigano nchini Somalia kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa hatari, kuwajibika na kusimamia mabaki ya silaha za kivita kwa utaratibu maalum, na kuondoa mabomu yaliyotegwa ardhini yaliyopo sasa na vifaa vingine vyovyote vya mlipuko.
Wakati huo huo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia lilichukizwa na shambulio hilo “la kuogofya” ambalo limelilaumu kundi la Kiislamu lenye itikadi kali la Al Shabaab.
Wanachama hao wamesisitiza tena msimamo wa Baraza la kulaani ugaidi “kwa kila aina na udhihirisho wake” kama moja ya matishio makubwa kwa amani na usalama wa kimataifa na kutaja vitendo vyote vya kigaidi kuwa “uhalifu na visivyoweza kuhalalishwa bila kujali motisha yao.”
“Kwa kweli hii ni siku mbaya na ya kutisha kwa UNICEF, na kwa wale wote ambao wenzetu hawa walikuwa wakifanya kazi kwa ajili yao nchini,” Edward Carwardine, Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano wa UNICEF katika mahojiano na Redio ya Umoja wa Mataifa.
Alisema UNICEF imekuwa Somalia tangu mwaka 1972 na mipango yake sasa inalenga hasa maeneo kama vile maji, elimu, lishe ya afya ya mtoto na ulinzi wa watoto. Shirika hilo, alisema “linafanya kazi kwa baadhi ya watoto na familia zilizo hatarini zaidi katika sehemu hiyo ya nchi.”
Na licha ya mkasa wa leo, Bwana Carwardine alisema, “Kazi inayoendelea ya UNICEF kwa watoto hawa walio katika mazingira magumu zaidi ni kipaumbele chetu na tumejitolea kuendeleza hilo kadri tuwezavyo.”