Wizara ya elimu ya Morocco imesitisha kwa muda kujifunza kwa wanafunzi katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi na tetemeko la ardhi.
Ilisema Jumapili kwamba inatafuta njia ambazo wanafunzi wanaweza kuendelea kujifunza huku mikoa yao ikipata nafuu.
Wizara hiyo iliongeza kuwa kufikia sasa, walimu saba wanajulikana kufariki, huku wengine 39 wakipata majeraha.
Ilisema shule 585 ziliharibiwa na tetemeko la ardhi na wanafunzi wengine wanaweza kulazimika kuhamia shule tofauti.
Masomo yamesitishwa katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi na tetemeko la ardhi.
Wizara ilisema imeanzisha vikundi viwili vya “mgogoro” kusaidia kutathmini uharibifu na hali katika shule zilizoathiriwa.
“Wizara ya elimu ya taifa, shule ya awali na michezo inatoa pole kwa familia za marehemu na kuwatakia ahueni majeruhi, pamoja na wanafunzi wetu wapendwa ambao Wizara yao inashirikiana kwa dhati na machungu,” ilisema taarifa ya wizara hiyo. .