Ziara ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini katika kituo cha umeme Kihansi ambapo ziara hiyo imeongozwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Judith Kapinga.
Naibu Waziri wa Nishati amesema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi Bilioni 20 ili kufanya maboresho makubwa katika mabwawa ya umeme ya Kidatu, Kihansi na Mtera ili nchi iweze kuongeza ufanisi wa mitambo na hivyo iweze kutoa umeme wa uhakika.
Amesema kuwa vyanzo vyote vya umeme nchini vinafanya kazi kwa ufanisi lakini ifikapo februari 2024 majaribio ya uzalishaji umeme yataanza kufanyika katika Bwawa la Julius Nyerere na mwezi Juni 2024 uzalishaji umeme utaanza na hivyo kufanya nchi kuwa na umeme wa uhakika.