Eneo la Atlas ya Juu nchini humo lilikumbwa na tetemeko la ardhi la kipimo cha 6.8, ambalo limegharimu maisha ya zaidi ya watu 2,122 huku zaidi ya 2,421 wakijeruhiwa na wengine wengi kutoweka.
Ronaldo ametoa msaada wake kwa kufanya hoteli ya Pestana CR7 Marrakesh ipatikane kwa waathiriwa wanaotafuta hifadhi kutokana na janga hilo la asili.
Hoteli hiyo ya nyota nne ina vyumba 174 na inaonekana kama moja ya kumbi nzuri zaidi jijini na kwa kawaida hutoza karibu £130 kwa usiku.
Eneo la mji mkongwe wa Marrakesh limeathiriwa vibaya na tetemeko la ardhi na majengo na kuta kadhaa zimeanguka.
Wilaya hiyo inasifika kwa njia nyembamba ambazo hazipitiki kutokana na uharibifu huo.