Kuku kutoka shamba moja huko Michigan, ndiye anayeshikilia Rekodi ya Guinness kwa kuwa ‘kuku aliyeishi zaidi duniani’, akiwa na umri wa miaka 21, siku 156 na kuhesabika. lakini kikawaida kuku wana wastani wa kuishi miaka mitano hadi minane
Mnamo Januari 28, 2023, alitawazwa rasmi kuwa kuku mzee zaidi duniani na Guinness World Record, akiwa na umri wa miaka 20 na siku 272 na tangu wakati huo amefikisha umri wa miaka 21 na anawinda taji la kuku mkongwe zaidi katika historia iliyorekodiwa.
Lakini jambo la kushangaza zaidi kuhusu kuku Peanut ni kwamba miaka 21 iliyopita, mmiliki wake alikuwa akijiandaa kurusha kundi la mayai yaliyooza ambayo alikuwa ameyaacha muda mrefu aliposikia mngurumo hafifu kutoka kwa mmoja wao ambaye ndiye huyo sasa aliemuita peanut.
Darwin alisema kuwa alihimizwa kuomba rekodi ya Guinness kwa kuku wake na rafiki yake ambaye pia ni mpenda kuku kwani aliwahi kusikia kuhusu kuku anayeitwa Matilda ambaye hapo awali alikuwa ameshikilia rekodi hiyo akiwa na umri wa miaka 14, kisha akafa miaka michache baadaye.
Peanut alikuwa tayari ameshinda rekodi yake kwa miaka kadhaa, kwa hiyo alimshawishi Marsi kuomba, hata hivyo, kuthibitisha umri wa kuku sio jambo rahisi zaidi duniani.
“Nilikuwa na picha za tarehe za marafiki na wapwa ambao walikuwa wamepiga picha naye miaka iliyopita, kwa hivyo huo ulikuwa uthibitisho wetu bora,” Darwin alisema.