Mbunge wa Jimbo la Rorya Jafari Chege ameanza ziara kwa kutembelea makambi ya Umoja wa Vijana wilaya ya Rorya mkoa wa Mara, pamoja na mambo mengine Mbunge huyo ameshiriki katika shughuli za kimaendeleo akiwa na Wananchi wa Rorya.
Mbunge Chege pia ametoa fedha kiasi cha Tsh. 500,000 kwa vijana wapatao 180, ambao wako tayari kuanzisha kilimo cha kisasa na Uvuvi wa vizimba ili kujiinua kwa vijana wa Rorya.
“Mimi kama Mbunge wenu ni lazima niwatahadharishe vijana wengi wengine ni wadogo miaka 16 hadi 18, hawajajua siasa inavyochezwa, kwamba haya mambo ya watu kuzunguka kwenye majimbo na wengine kupotosha kuwahamisha kwenye mambo yasiyofaa tujitahadhari nayo” Mbunge Chege