Nyota wa Pop Joe Jonas alionekana kuzungumzia uvumi unaozunguka sababu za talaka yake kutoka kwa mwigizaji wa Uingereza Sophie Turner wakati wa tamasha la Jonas Brothers.
Jonas, 34, aliwasilisha talaka kutoka kwa Turner, 27, baada ya miaka minne ya ndoa mnamo 5 Septemba huko Miami Dade County, Florida.
Kulingana na hati za mahakama zilizopatikana na Today, ombi la talaka linasema kwamba “ndoa kati ya wahusika imevunjika kwa njia isiyoweza kurekebishwa”.
Huku kukiwa na ripoti kwamba ndoa yao ilikuwa imevunjika kwa sababu ya maisha tofauti ya Jonas na Turner, wanandoa wa zamani walitoa taarifa ya pamoja siku iliyofuata, kufafanua uamuzi wao wa talaka “baada ya miaka minne ya ajabu” ulikuwa wa kuheshimiana na wa kirafiki.
Mwimbaji huyo alikiri “imekuwa wiki ngumu” tangu talaka yao iliporipotiwa mara ya kwanza, wakati wa onyesho la hivi majuzi la Jonas Brothers kwenye Uwanja wa Dodgers huko Los Angeles Jumamosi (9 Septemba).
Akionekana kuzungumzia baadhi ya comment mbaya alizozipata kwenye mitandao ya kijamii, Jonas pia aliwataka mashabiki wasiamini chochote kuhusu uhusiano wao “ikiwa hawajasikia kutoka kwake “.
“Imekuwa wiki ngumu. Ninataka tu kusema, angalia, ikiwa hausikii kutoka kwenye midomo hii, usiamini. Sawa?” Jonas alisema.
“Asante kila mtu kwa upendo na msaada wako. Mimi na familia yangu tunawapenda ninyi.”
Wiki iliyopita, TMZ iliripoti Turner na Jonas – ambao wana watoto wawili pamoja – walikuwa wakimalizia talaka, baada ya miezi sita ya “matatizo” katika uhusiano wao.