Mahakama ya Juu ya Israel imeanza kusikiliza kesi inayolenga kupinga kipengele kikuu cha marekebisho ya sheria yenye utata ya serikali ya mrengo wa kulia ambayo yamesababisha maandamano makubwa na kuligawa taifa hilo.
Jopo la majaji 15 wa mahakama ya juu limekutana kusikiliza maombi ya kupinga kubadilishwa kwa kile kinachoitwa kifungu cha busara ambacho serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ilipitisha bungeni mwezi Julai.
Serikali yake waziri wa sasa Benjamin Netanyahu ilipitisha marekebisho ya katiba kwa kura 64 bila ya upinzani kwenye bunge la Israeli.
Haya yanajiri wakati huu maandamano yakidumu kwa zaidi ya miezi tisa tangu kuanza kwa mchakato huo januari mwaka huu.
Marekebisho hayo yanayopendekezwa yanaweka ukomo wa mamlaka ya mahakama ya juu kupitia upya na wakati mwingine kubatilisha maamuzi ya serikali, ambayo wapinzani wanasema yanafungua njia kwa utawala wa kimabavu.
Tangu kuzinduliwa kwa mipango hiyo ya serikali Januari mwaka huuu ,makumi kwa maelfu ya wapinzani wameandamana katika miji yote kutaka sheria hiyo kutupiliwa mbali.
Usiku wa kuamkia leo raia wameandamana huku wakiimba democrasia.