Utawala wa Biden umefanya makubaliano na Iran kuachilia dola bilioni 6 kama fedha zilizohifadhiwa ili kubadilishana na kuachiliwa kwa wafungwa watano wa Kimarekani nchini Iran kwa kutoa msamaha kwa benki za kimataifa kuhamisha dola bilioni 6 za pesa za Iran zilizohifadhiwa kutoka Korea Kusini hadi Qatar bila woga wa vikwazo vya Marekani.
Aidha, ikiwa ni sehemu ya makubaliano hayo, utawala huo umekubali kuwaachilia huru raia watano wa Iran wanaoshikiliwa nchini Marekani.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alitia saini makubaliano ya kuondolewa kwa vikwazo mwishoni mwa wiki iliyopita, mwezi mmoja baada ya maafisa wa Marekani na Iran kusema kwamba makubaliano kimsingi yapo.
Congress haikufahamishwa juu ya uamuzi wa msamaha hadi Jumatatu, kulingana na arifa hiyo, ambayo ilipatikana na The Associated Press.
Muhtasari wa mpango huo ulikuwa umetangazwa hapo awali na msamaha ulitarajiwa lakini arifa hiyo iliashiria mara ya kwanza kwa serikali kusema inawaachilia wafungwa watano wa Iran kama sehemu ya makubaliano hayo,wafungwa hao hawajatajwa.
Mwezi uliopita wafungwa wanne kati ya watano walihamishwa kutoka jela za Irani na kupelekwa katika kifungo cha nyumbani katika hoteli katika mkataba huo wenye utata unaoelezewa kama noti ya fidia ya wakosoaji wa chama cha Republican.
Msamaha huo unamaanisha kuwa benki za Ulaya, Mashariki ya Kati na Asia hazitaenda kinyume na vikwazo vya Marekani katika kubadilisha fedha zilizohifadhiwa nchini Korea Kusini na kuzihamishia katika benki kuu ya Qatar, ambako zitashikiliwa kwa ajili ya Iran kuzitumia kwa ununuzi wa bidhaa za kibinadamu. .