Kiongozi wa chama cha wa Republican katika Baraza la Wawakilishi la Marekani, Kevin McCarthy, ameomba Jumanne hii, Septemba 12, kufunguliwa kwa uchunguzi kwa nia ya uwezekano wa kesi ya kuondolewa madarakani kwa rais Joe Biden kutoka chama cha Demokrat.
Mwakilishi wa chama cha Republican katika Bunge la Congress anabaini kwamba Joe Biden “alidanganya” raia wa Marekani kuhusu masuala yenye utata ya mtoto wake nje ya nchi.
Hunter Biden, mtoto wa miaka hamsini wa rais wa Marekani, analengwa na mrengo wa kulia wa Marekani. Wanamtuhumu hasa kwa kufanya mikataba yenye shaka nchini Ukraine na China wakati Joe Biden aalipokuwa makamu wa rais wa Barack Obama (2009-2017), akitumia mitandao na jina la babake.
Ikiwa imeigizwa katika Katiba ya Marekani kama hatua ya mwisho, kushtakiwa kwa rais imekuwa kama silaha ya kisiasa. Baada ya majaribio mawili ya wabunge na maseneta wa chama cha Democratic ya kumshtaki Donald Trump, mwaka wa 2019 na 2021, yaliyopigiwa kura na Baraza la Wawakilishi, lakini kukataliwa na Bunge la Seneti, Warepublican sasa wanataka kulipiza kisasi kwa kuchukua hatua sawa dhidi ya Joe Biden.
Mrengo mkali wa chama katika Bunge la Congress unashinikiza kufunguliwa kwa kesi ya mashtaka dhidi ya rais Joe Biden kutoka chama cha Democratic, ambaye inamtuhumu kwa ufisadi.