Katika kukuza sekta ya utalii Wilayani pangani Mkuu wa wilaya hiyo Zainab Abdallah amesema kuwa amedhamiria kukuza sekta hiyo kwa kuhakikisha makundi ya vijana na pamoja na wawekezaji wana nufaika na rasilimali za utalii zilizopo ,jambo ambalo litasaidia kufungua uchumi wa wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya muda mfupi ya utalii yaliyotolewa kwa siku sita kwa vijana 51 wa wilaya hiyo kutoka chuo cha Taifa cha Utalii kwa kushirikiana na wakufunzi wa ndani.
Aidha Dc Zainab amesema amedhamiria kufungua wilaya ya pangani kupitia kampeni yake ya WEKEZA PANGANI kwa kushirikisha makundi mbalimbli ya Vijana,Wanawake,Wazee pamoja na wawekezaji kupitia sekta ya Utalii,Kilimo na Biashara (Agro Business) sambamba na Uchumi wa Bluu (Bluu Economy) ambayo ni agenda ya Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassani na Rais wa Zanzibar Mhe.Dkt Hussein Mwinyi.
Kwapande wake mkuu wa chuo cha Utalii Dkt.Florian Mtei amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha juhudi kubwa zinazo fanywa na Mkuu wa wilaya ya panganiya kuwainua vijana kiuchumi kupitai sekta ya utalii wanaziunga mkono katika kuhakikisha jamii ya wanapangani wana nufaika na Rasilimali zilizopo katika maeneo yao.